Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki waiponza Yanga, yalimwa faini

Yanga Mashabiki Ks Mashabiki waiponza Yanga, yalimwa faini

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Sh1 milioni kwa kosa la mashabiki wake kurusha chupa za maji kiwanjani baada ya timu ya Ihefu kufunga bao la pili.

Katika mechi hiyo iliyopigwa uwanja wa Highland Estate mkoani Mbeya, Ihefu ilishinda mabao 2-1.

Yanga pia imetozwa Sh1 milioni kwa kosa la maofisa wa benchi la ufundi kuonekana wakipinga maamuzi ya waamuzi wa mchezo huo na kumzonga mwamuzi wa akiba.

Makosa hayo yameainishwa katika taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu iliyotolewa leo Oktoba 19 baada ya kikao cha maamuzi kuketi jana.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya bodi hiyo iliyosambazwa kwa vyombo vya habari leo Alhamisi Oktoba 19. 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: