Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki waibeba Coastal Union

Coasta Union FC Tanga Kikosi cha Coastal Union

Sat, 11 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Katibu Mkuu wa Coastal Union, Omary Ayoub amesema ili klabu hiyo iweze kunufaika kiuchumi na uwingi wa mashabiki wao ni jukumu la kuwaandaa wachezaji wenye ushindani wa kupata matokeo ya ushindi.

Alifafanua kauli yake kwamba timu inaposhinda mashabiki wanakuwa wananunua jezi kwa wingi, akitolea mfano msimu uliopita kwamba ziliuzwa takrabani 10,000.

“Ukiondoa Simba na Yanga, Coastal Union ni timu ya tatu kwa utajiri wa mashabiki, ili tunufaike nao ni timu kufanya vizuri ndipo wanapojitokeza kwa wingi uwanjani na kununua jezi.

“Mbali na jezi timu inapopata matokeo ya ushindi wanachama wanahamasika kulipa ada ya uanachama kila mwezi, ndio maana wachezaji wapya wanapojiunga na timu huwa wanashangaa kukutana na presha ya mashabiki.”

Mbali na hilo, katibu huyo alisema wingi wa mashabiki na timu kufanya vizuri kunawavutia wawekezaji, kwani inakuwa fursa kwao kutangaza biashara za wawekezaji hao, Simba na Yanga zisingekuwa na mashabiki sidhani kama zingekuwa na wadhamini walionao.”

Chanzo: Mwanaspoti