Mashabiki na wapenzi wa wana lamba lamba Azam FC wamesikitishwa na kitendo cha uongozi wa klabu nhiyo kumuongezea mkataba kocha mkuu wa kikosi hich Mzambia George Lwandamina.
Mapema mwanzoni mwa juma hili taarifa zilitoka kwamba Kocha huyo ameongeza mkataba ndani ya kikosi hicho licha ya mfululizo wa matokeo mabaya waliyoyapata siku za hivi karibuni.
Azam wametolewa Kombe la Shirikisho na FC Pyramids, na wakapoteza jumamosi iliyopita mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga.
Sasa walio wengi wanaona uongozi umeshindwa kuwajibika kwa namna mwenendo wa timu ulivyo mpaka sasa.
"Azam wana kila kitu,uwekezaji wao ni mkubwa "level" za kina Simba na Yanga lakini kila msimu tunazidiwa sasa hapo unadhani tatzo ni nani kama sio kocha halafu etileo mtu anakuja anajitapa kumuongezea mkataba huu uongozi wa hovyo kabisa" amelalama shabiki huyo
wakati wengine wamekwenda mbali na kudai viongozi wanaitumia Azam kwa manufaa yao na hasa Mtendaji Mkuu Abdulkarim Amin 'Popat'.
"Hawa wengine ni mamluki tu ndio wanaotumwa na timu za kariakoo kuja kuidhoofisha Azam, we jinsi unavyoona timu ya Azam ni ya kushindwa kubeba ubingwa miaka yote hii? sio kweli na haingii akilini hwa viongozi ni wapigaji tu wanampiga hela mwenye timu"
Kocha George Lwandamina, ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuwa Kocha wa Azam, Novemba Mosi, kwenye ukumbi wa wageni maalumu ndani ya uwanja wa Azam Complex, mbele ya Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat'.
Alijiunga na Azam Novemba mwaka jana na hadi sasa ameiongoza timu hiyo katika mechi rasmi 37 za mashindano yote.
Ligi Kuu michezo26, ASFC michezo minne (4), Mapinduzi Cup michezo mitatu (3), Shirikisho Afrika michezo minne (4).