Baada ya Kikosi cha Yanga kuanza msimu wa ligi vivuri kwa kuiadhibu KMC kwa bao 5-0, mashabiki wa timu hiyo wameshindwa kujizuia na kuonyesha mahaba yao ya wazi kwa kiungo wao, Pacome Zouzoua aloyesajiliwa msimu huu kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast.
Pacome Zouzoua, ni saa 5:50 usiku kwa saa za ardhi ya Mwalimu Julias Nyerere! Natamani angelikuwepo mwalimu Kashasha nione uchambuzi wake kwa MVP wa Ivory Coast akiwa kwa giants wa soka la Bongo ambao ni Yanga.
Naupenda sana mpira, nahusudu sana mbinu za mwalimu Miguel Gamondi kwa kumpa nafasi zaidi Pacôme Zouzoua atashinda mechi zake nyingi hapa! Pacôme Zouzoua ana spirit kama Zinedine Zidane.
Mwaka 1998 kwenye dunia ya mpira wa miguu ilikuwa inaona burudani kwa Zinedine Zidane! Wakati mwaka 2023 kwenye mpira wa miguu tuna shuhudia burudani za Profesa wa mpira ambae ni Pacôme Zouzoua, unapitia hili andiko huoti upo macho.
Ni umbali wa 4,746 kilometers ambao YANGA ilisafiri kwenda Ivory Coast kumpata PACÔME ZOUZOUA! Top top player, haikuwa kwa ajili ya usajili wa Wananchi bali kusajili Mchezaji wa dakika 90 na sio kama wachezaji wengine, sifanyi Hip-hop siwezi taja majina.
YANGA kwenye game hii sio tishio katika kushinda Makombe tu hadi kusajili! PACÔME ZOUZOUA ataisaidia sana YANGA, hata namna alivyo na kijiji chake kwao Ivory Coast ni dhahiri kuwa ni Top top Professional.