Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wa Yanga wanamatumaini CAFCC

YANGA 10 Mayele Yanga watacheza Fainali na USM Algier

Sun, 21 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa Yanga mkoani Mbeya wameonesha matumaini ya timu hiyo kubeba ubingwa wa kombe la shirikisho Afrika huku wakieleza safari yao kwenda Dar es Salaam kuisapoti kwenye mchezo wao wa fainali dhidi ya USM Algers.

Yanga unatarajia kushuka uwanjani Mei 28 katika mchezo wa fainali hiyo ya kwanza dhidi ya wapinzani hao kabla ya kurudiana nao Juni 3 nchini Algeria.

Yodi Mhagama mwanachama wa timu hiyo jijini hapa amesema wanayo matumaini makubwa kwa timu hiyo msimu huu kuweka historia ya kuleta taji hilo la Afrika nchini.

Naye Zuhura Hamza amesema pamoja na maandalizi yao ya kuishangilia timu hiyo katika mechi ya fainali ya kombe la shirikisho Afrika, lakini wanajiandaa na mapokezi ya timu hiyo jijini hapa kwa ajili ya mechi zao za ligi Kuu dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons.

Naye Jackson Michael 'Jackpemba' amesema msimu huu Yanga haiachi kitu na wanaanza na Singida Big Stars kesho Jumapili kisha kuigeukia USM Algers.

Bedom Mwambogolo amesema Yanga ya sasa haifananishwi na mwaka mwingine wowote na kwamba hii ni tishio kila sehemu, huku akishangiliwa na mashabiki wenzake.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: