Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wa Yanga wamtoa kwenye mikono ya polisi GB64

GB64 WA0015 Mashabiki wa Yanga wamtoa kwenye mikono ya polisi GB64

Sun, 21 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanachama wa Klabu ya Simba maarufu kama GB64 hii leo ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na Polisi kabla ya mchezo wa watani wa jadi kwa kile kilichoelezwa kutoa kauli za uchochezi.

Mwanachama wa Klabu ya Young Africans maarufu Mwalimu Yanga ndie amemwekea dhamana mchana wa leo na pia kumkabidhi kiasi cha pesa Tsh 100,000 iliyochangwa na wadau wengine.

GB64 amekabidhiwa pia simujanja (smartphones) mbili na mashabiki hao ambazo aliwahi kuomba achangiwe ili aachane na matumizi ya kiswaswadu (simu kitochi).

Hongera Mwalimu Yanga kwa hili, Mpira sio uadui.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live