Mpira wa Tanzania unazidi kukua kwa kasi, asilimia kubwa ya mashabiki wa Simba wakihojiwa unaona kabisa wanaongea uhalisia wa mpira kuliko zamani wengi wanasema na wanaamini wamefungwa kwa sababu ya ubora wa wachezaji wa Yanga kuliko wao.
Hii ni hatua kubwa sana kwa mpira wetu ingekuwa zamani hata timu ifungwe vipi utawasikia wanalaumu kurogwa, waaamuzi, viongozi au kocha ni asilimia ndogo sana ya mashabiki wa Simba inayoomini wamefungwa kwa uzembe wa viongozi wao.
Pamoja na Simba kufungwa bado mashabiki wana imani na kocha wao (Benchikha) ni mara chache sana Derby ya Simba na Yanga kuisha na timu iliyofungwa isimulaumu kocha ila Derby ya juzi mashabiki wa Simba wanaamini ubora wa Yanga ndio umewafanya wapoteze mechi.
Hii ni nuru sana kwa TFF na TPLB tunaendelea kubadilika kila siku zamani kwenye mechi za Simba na Yanga zilikuwa vita na hekaheka sana huwezi kukuta mashabiki wa Simba na Yanga wanakaa pamoja Ila kwa sasa unakuta kundi la mashabiki wa Yanga ndani ya Simba wanaenjoy football tunaendelea kuelimika.
Tulikuwa tunawashangaa Wazanzibar wanawezaje mashabiki wa Simba na Yanga kukaa pamoja na hamna vita yoyote? Ila kwa sasa Tanzania bara tumeweza na sisi, Hongera pia Arajiga, Mkono, Mpanga na Tatu Malogo kwa kazi kubwa mliyoifanya jan kuitendea haki Derby hakuna malalamiko sana juu ya waamuzi wa mchezo wa jana wametenda haki bin haki.
Tunapoelekea mwisho wa misimu ya ligi nawatakia kila la kheri viongozi wetu wa TFF na TPLB kuendelea na weredi huu wa usimamizi kwenye ligi zetu, Tanzania imepata Rais wa mpira Hongera mingi sana Karia umeyafanya yasiyowezekana yakawezekana Tanzania hatimaye tunazidi kuelimika.