Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wa Simba wafungiwa miezi 6

Shabiki Wa Yanga Aliepigwa Mkapa Mashabiki wa Simba wafungiwa

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imewafungia kwa miezi sita kuingia viwanjani kwenye michezo ya michuano yote ya TFF, mashabiki wanne walioonekana kupitia video kwenye mitandao ya kijamii wakimshambulia shabiki mmoja aliyekuwa amevaa jezi ya klabu ya Yanga katika mchezo tajwa hapo juu.

Kupitia taarifa yake kwa umma TPLB imewataja Mashabiki hao kuwa ni Hassan Khatibu, Hamza Dafa, Patrick Shelukindo na Shaban Anga ambao walifanya tukio hilo katika mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Ihefu FC uliomalizika kwa Simba kushinda 2-1.

Bodi imewataka mashabiki kujiepusha na vitendo vya vurugu na kupigana viwanjani ili kudumisha upendo na umoja michezoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live