Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wa Simba mjiandae kisaikolojia - Amri Kiemba

Karaboue Chamou.jpeg Mashabiki wa Simba mjiandae kisaikolojia - Amri Kiemba

Mon, 8 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa Soka, Clouds FM kipindi Hili Game, Amri Kiemba amesema kutokana na usajili walioufanya Klabu ya Simba kwa kuwaondoa nyota wengi na kuleta wachezaji wengi wapya, uwezekano wa kuchukua ubingwa msimu huu utakuwa mgumu.

Simba mpaka sasa wamesajili wachezaji 10 ambao ni Deborah Fernandez, Valentino, Mashaka, Karaboue Chamou, Omar Omar, Abdulrazak Hamza, Augustine Okejepha, Cahrlels Jean Ahoua, Joshua Mutale, Steven Mukwala na Valentino Nouma.

“Simba ni kama wameamua kusafisha nyumba na kuweka furniture mpya , hata usajili wao tutegemee utakuwa mkubwa.

“Bahati mbaya sana viwango vya timu zingine vimekuwa sana kwa hiyo wanatakiwa kuleta watu wenye uwezo mkubwa wa ushindani.

“Matarajio hayapaswi kuwa makubwa sana kwenye msimu huu ambao timu imeanza kujitengeneza kwa sababu sayansi inakataa.

“Mashabiki wajiandae kisaikolojia ili hata wakikosa ubingwa kelele zisiwe nyingi,” amesema Amri Kiemba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live