Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wa Simba kuwa wageni rasmi dhidi ya ASEC Mimosas

Mashabiki Wa Simba Kuwa Wageni Rasmi Dhidi Ya ASEC Mimosas Mashabiki wa Simba kuwa wageni rasmi dhidi ya ASEC Mimosas

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema mashabiki wao ndio watajaokuwa wageni rasmi katika mchezo wao wa kwanza wa hatua ya Makundi dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Novemba 25, 2023.

Ahmed ameyasema hayo leo Novemba 16, 2023 alipokuwa akitangaza ratiba yao kuelekea mchezo huo mkubwa utakaopihgwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

“Wageni rasmi wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas watakuwa ni mashabiki wa Simba. Kwanza wametoka kushinda tuzo ya mashabiki bora hivyo kila Mwanasimba akija siku hiyo ajue yeye ni mgeni rasmi.”

“Tusahau yaliyopita na tuangalie mbele. Huu ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa tukipoteza na tukiwa nyumbani hatutakuwa kwenye sehemu nzuri ya kwenda hatua ya mbele. Twendeni tukawape moyo wachezaji wetu kwamba tunaanguka pamoja na kusimama pamoja."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live