Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wa Simba kupewa chakula, vinywaji Kwa Mkapa

Simba Nm.jpeg Mashabiki wa Simba kupewa chakula mechi ya Raja Casablanca

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiingilio cha chini ya mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Februari 18 kitakuwa Sh. 5000.

Viingilio vimetangazwa mapema ili kuwapa nafasi mashabiki kununua mapema sababu ya mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu.

Viingilio ni kama ifuatavyo:

Mzunguko Sh. 5000

VIP B & C Sh. 20000

VIP A Sh. 30,000

Platinum Sh. 100,000

Platinum Plus Sh. 150,000

Vitu ambavyo atavipata atayenunua tiketi za Platinum ni.

1. Escort kutoka Hoteli ya Hyatt Regency mpaka uwanjani.

2. Kifurushi maalum kutoka Simba.

3. Chakula na Vinywaji ukiwa uwanjani.

Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwa njia ya mtandao muda mfupi ujao vitatangazwa vituo ambavyo zitapatikana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live