Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wa England waonywa Bia za Ujerumani Euro 2024

Mashabiki Boa Ujerumani Mashabiki wa England waonywa Bia za Ujerumani Euro 2024

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wa soka kutoka Uingereza watakaokwenda Ujerumani kwenye michuano ya Euro wameonywa kuwa bia nchini Ujerumani zina nguvu zaidi kuliko za Uingereza.

Mashabiki wa England na Scotland wameambiwa kuwa watazuiwa kuingia uwanjani iwapo wataonekana kuwa wamelewa sana.

Wizara ya mambo ya nje imetoa angalizo hilo kabla ya kuanza kwa michuano hiyo itakayofanyika mwezi Juni na Julai.

“Bia inaweza kuwa kali kuliko ya Uingereza, kwa hiyo kunywa kistaarabu, fahamu kikomo chako na uheshimu sheria za nchi,” limesema angalizo hilo.

“Unaweza kuzuiwa kuingia uwanjani ukinywa kupindukia”.

Maelfu ya mashabiki kutoka Uingereza wanatazamiwa kwenda kwenye michuano hiyo ambayo itafanyika katika miji kumi ya Ujerumani.

Wastani wa nguvu ya kilevi ya bia ya laga nchini Uingereza ni takriban asilimia 4.4, kwa mujibu wa shirika la Drinkaware.

Bia za Ujerumani zinaweza kuwa kati ya asilimia 4.7 na 5.4.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live