Mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji Esperance ya Tunisia dhidi ya JS Kabylie ya Algeria ulilazimika kusimama kwa muda jana baada ya umati kuleta vurugu katika dimba la Olympique Hammadi Agrebi Mjini Rades, Tunisia.
Hii ilitokana na vurugu za mashabiki wa Esperance baada kuwasha moto na moshi kufuka uwanja mzima huku wachezaji wa Kabyle wakikimbilia vyumbani ili kujihami maisha yao.
Mpaka mwisho wa mchezo, Esperance wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kabyle hukuwa matokeo ya jumla yakiwa ni bao (Esp 2-1 Kab) ambayo yamewapa nafasi Esperance kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya kombe la Mabingwa Afrika.
Esperance sasa watakutana na Al Ahly ya Misri ambayo ilifanikiwa jana kutinga nusu fainali kwa kuiondoa Raja Casablanca ya Morocco.
Kwa vuru hizo za mashabiki wa Esperance huenda klabu ikapigwa faini na adhabu nyingine kubwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).