Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wa Arsenal wa Kenya watoa shukrani kanisani baada ya ushindi

Mashabiki Wa Arsenal Wa Kenya Watoa Shukrani Kanisani Baada Ya Ushindi Mashabiki wa Arsenal wa Kenya watoa shukrani kanisani baada ya ushindi

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Mashabiki wa Arsenal katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, walikusanyika katika kanisa la mtaani kwa kipindi maalum cha maombi, ili kuonyesha shukrani baada ya timu yao kuwalaza Crystal Palace 5-0 katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Uingereza Jumamosi.

Wakiwa wamevalia mashati ya Gunners, mashabiki hao waliimba kwa furaha na kutoa shukrani kwa uchezaji mzuri wa timu yao wakati wa ibada ya Jumapili asubuhi.

Pia walitoa maombi wakitumaini kuendelea kupata mafanikio kwa Arsenal katika msimu unaoendelea.

Mwanahabari Kennedy Muriithi, ambaye alikuwa miongoni mwa waliohudhuria, alisambaza picha za ibada ya maombi kwenye mitandao ya kijamii

Arsenal kwa sasa wanalingana pointi na Manchester City, ambao wana mchezo mkononi dhidi ya timu hiyo ya Kaskazini mwa London, na pointi tano nyuma ya Liverpool walio kileleni mwa jedwali.

Picha hizo zilizua hisia tofauti kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi wakikejeli mashabiki.

Chanzo: Bbc