Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki ulaya waigomea Uefa

Gfrdfcxfx Mashabiki ulaya waigomea Uefa

Sun, 14 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Inawezekanaje? Ndicho wanachohoji mashabiki wa soka baada ya Shrikisho la Soka Ulaya (Uefa) kutoa taarifa ya viwango vya ubora wa klabu za bara hilo na kudai haina uhalisia.

Utata umeibuka baada ya Manchester City licha ya kushindwa kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, imeendelea kuwa ya kwanza huku Real Madrid iliyobeba taji hilo ikishika nafasi ya pili.

Kwenye taarifa hiyo, utata mwingine ni nafasi ya tatu inayoshikiliwa na Bayern Munich na kilichowashangaza mashabiki ni miamba hiyo ya Bundesliga licha ya kutokufanya vizuri msimu uliopita na kupoteza ubingwa wa ligi mbele ya Xabi Alonso na Bayer Leverkusen yake, imeshika nafasi hiyo.

Pia taarifa hiyo inaonyesha Majogoo wa Anfield, Liverpool na AS Roma zimefunga nafasi tano za juu kwa kushika nafasi ya nne na tano mtawalia, huku Mashetani wekundu, Manchester United ikitupwa hadi nafasi ya 14.

Arsenal iliyomaliza nafasi ya pili Ligi Kuu England msimu uliopita baada ya kuwa kwenye nafasi nzuri ya kubeba taji hilo kabla ya kupinduliwa na Man City, imekamata nafasi ya 19, huku West Ham iliyofanya vizuri michuano ya kimataifa msimu uliopita ikishika nafasi ya 16.

Baada ya taarifa ya viwango hivyo kutoka, mashabiki katika mitandao ya kijamii waliwaka na kuonyesha kutoridhishwa nayo.

Mmoja aliandika: “Haiwezi kuwa sawa, yaani Man City iwe juu kuliko Madrid.”

Mwingine akasema “Inawezekanaje, Chelsea iwe juu ya Barcelona, haya ni masihara.”

Kwa mujibu wa Uefa wenyewe, viwango hivi vya ubora vimezingatia mafanikio ya timu katika michuano ya kimataifa kwa misimu mitano iliyopita.

Kwa hivyo, West Ham ambayo ilifika nusu fainali ya Europa League msimu wa 21/22 na kushinda Conference League mwaka uliofuatia imejikusanyia pointi nyingi zaidi kuliko Arsenal na Barcelona.

Chanzo: Mwanaspoti