Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki ruksa mechi ya Stars kesho

Ed 8WY2XoAAYkup Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeruhusu mchezo baina ya Taifa Stars na Benin kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuingia mashabiki wasiozidi 10,000

Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema kuwa wamepokea taarifa hiyo kutoka CAF wakiruhusiwa kuingiza namba hiyo ya mashabiki katika mechi hiyo ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia

“Tumepata taarifa hii kwa kuchelewa lakini sio sababu ya mashabiki kushindwa kuja kuisapoti timu yao. Watu 10,000 ni wengi lakini kulingana na ukubwa wa Uwanja wa Mkapa ni wachache hivyo tunawaomba wajitokeze kwa wingi,” amesema Ndimbo

Awali taarifa zilidai kuwa mashabiki hawatoruhusiwa kuingia uwanjani katika mechi hiyo na hiyo ilitokana na kuchelewa kwa CAF kurudisha majibu ya ombi la TFF la kuruhusiwa kuingiza mashabiki.

Viingilio katika mchezo huo ni shilingi 3000/= kwa mzunguko na 5000/= kwa VIP B&C

Chanzo: www.tanzaniaweb.live