Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki msiifananishe Simba na Yanga - Jemedari Said

Ajibu Chama Mashabiki msiifananishe Simba na Yanga - Jemedari Said

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi maarufu wa masuala ya Soka nchini, jemedari Said Bin Kazumari ameonyesha kushangazwa na baadhi ya mashabiki wa Simba SC ambao wamekuwa wakilalamika kuwa timu yao haichezi vizuri.

Jemedari amesema hayo mara baada ya kumalizka kwa mchezo wa raundi ya tatu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union ambapo Simba walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 3-0.

"Simba imecheza mechi 3 za Ligi Kuu imeshinda zote imefunga mabao 9 imefungwa 2 ina alama 9, imecheza mchezo 1 wa Ligi ya mabingwa ugenini dhidi ya Power Dynamos imetoka sare 2-2 mchezo wa marudiano ni tarehe 1.10.2023 Chamazi.

"Yanga imecheza mechi 3 za Ligi kuu imeshinda zote ina alama 9 imefunga mabao 11 imefungwa bao 1, imecheza michezo 3 ya Ligi ya mabingwa ikianza hatua ya awali ambako walicheza na Asas ya Djibouti ambako mechi zote zilichezwa Chamazi kabla ya kuifunga El Merreikh ya Sudan 2-0 mchezo ukichezwa Kigali Rwanda.

"Pamoja na matokeo mazuri ambayo Simba inayapata lakini bado mashabiki wa Simba wanaonekana hawana furaha wanataka timu yao ishinde mabao tano tano kama Yanga, ishinde mechi ya ugenini kwenye Champions League kama Yanga, etc etc etc.

"Wanasahau mpira hauko namna hiyo, Simba inapaswa kupimwa kwa kiwango chake cha nyuma kuliko kuifananisha na Yanga huku factors nyingi hawalingani.

"Mjadala umekuwa Simba haichezi kama Yanga kuliko kuiangalia Simba yenyeewe kwa kile inachokipata kuna muendelezo mzuri kuelekea ubora wake? Maingizo mapya 13 kwenye kikosi cha Simba msimu huu haiwezi kuwa rahisi kucheza sawasawa na Yanga ambayo haijabomoka sana na ile iliyochukua Back-to-Back Ligi kuu huku msimu mmoja ikiwa haijapoteza mchezo hata 1 na ikicheza fainali ya CAF.

"Yanga ndiyo top performers kwenye mpira wa Tanzania kwa sasa kama ilivyokuwa Simba misimu kadhaa nyuma. Kile kiwango chao ndiyo inapaswa kuwa kipimo na sio kuitaka kucheza kama Yanga.

"Mashabiki wa Simba badala ya kuitaka timu yao kucheza kama Yanga na kuungana na mashabiki wa wapinzani wao kuizodoa timu, wanapaswa kujua wametoka kwenye ubora sasa wanajitafuta kuelekea ubora na Yanga wao wako kwenye ubora. Huu mchakato sio wa msimu 1 ni Kwani sio jambo rahisi, wakumbuke Yanga walikotoka na akina Balinya, Sarpong, Yikpe etc etc na walipo sasa.

"Binafsi naona Simba wanaenda vyema kuelekea kwenye ubora, kwa sasa wanakosa baadhi ya vitu lakini hawako mbali na ukweli ni suala la kuungana na kusapotiana wao kwa wao mwisho WATAJIPATA," amesema Jemedari Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: