Baada ya Klabu ya Yanga kuruhusu mashabiki zao kuingia bure kwenye mchezobwao wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns katika Dimba la Mkapa, ASP Hashim Abdallah, Mkuu wa Usalama Viwanjani TFF, CAF na FIFA amefunguka haya;
"Inapotokea mechi za bila vingilio [bure] huwa natoa ushauri kwa sababu jambo hili lina upana na uzito wake, wakati wa utawala wa Manji kuna mechi ilikuwa bure [Yanga vs TP Mazembe] tulipiga mabomu mengi sana ya machozi.
"Uwanja ulijaa tukafunga mageti, zikaibuka vurugu ndicho kilichotokea juzi [Yanga vs Mamelodi Sundowns]. Viongozi wanatakiwa wajifunze, inawezekana wana nia njema watu washuhudie mechi lakini kiusalama inakuwa ni shida kubwa.
"Mechi ya juzi [Yanga vs Mamelodi Sundowns] mimi nilisimamia watu kuingia uwanjani mapema, saa 4 asubuhi nje ya uwanja kumejaa, watu wapo magetini wanataka kuingia ndani mechi ya saa 3 usiku!
"Tukaongeanao kisiasa ikashindikana tukaanza kuwaruhusu kuingia, mpaka saa 9 alasiri watu bado wanaingia. Nikaamuru kufunga uwanja.
"Naamini hili limekuwa fundisho kwetu watu wa usalama na viongozi wa klabu kwamba wanapotoa kauli wahakikishe wamejipanga kulingana na aina ya viwanja vyetu na watu tulionao."