Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki Yanga wawafunika Marumo

IMG 4094.jpeg Mashabiki Yanga wawafunika Marumo

Wed, 17 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ukifika hapa uwanja wa Royal Bafokeng, Rustenburg, Afrika Kusini itakapopigwa mechi ya nusu fainali ya pili, Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Marumo Gallants na Yanga unaweza kusema ‘Wananchi’ ndio wako nyumbani kutokana na wingi na vaibu lao.

Ikiwa imebaki nusu saa kuanza kwa mechi hiyo itakayopigwa kuanzia saa 12:00 za hapa Afrika Kusini sawa na saa 1:00 za Tanzania, mashabiki wa Yanga wameonekana kuwa wengi kuliko wenyeji.

Mashabiki hao wa Yanga ambao kwa makadirio ni kama 1,000 hadi 2,000 wamekaa kwenye jukwaa moja wakiendelea kushangilia huku wale wa Marumo wakiwa hawafiki hata 3,00.

Wengi wa mashabiki hao wa Yanga wametokea hapa Afrika Kusini katika miji yofauti huku wengine wakitokea nchi za jirani na wengine Tanzania.

Yanga inahitaji ushindi au sare yeyote ili kufuzu fainali baada ya mechi ya kwanza nyumbani Dar es Salaam kushinda 2-0.

Chanzo: Mwanaspoti