Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki, Wanachama Simba SC watulizwa

Mashabiki Simba SC AS VITA 1140x640 Mashabiki na Wanachama wa Klabu ya Simba SC

Thu, 5 Jan 2023 Chanzo: dar24.com

Mashabiki na Wanachama wa Klabu ya Simba SC wameombwa kuwa watulivu na kuuamini Uongozi wao katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili, ambacho kimekua na Tetesi nyingi kupitia Mitandao ya Kijamii.

Simba SC imekua ikitajwa sana katika Mitandao ya Kijamii kwa kuhusishwa na Mipango ya Usajili wa baadhi ya Wachezani Wazawa na wale wa Kimataifa, lakini Uongozi umekua ukiwataka Mashabiki na Wanachama wake kuwa watulivu.

Safari hii ombi kwa Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo limetolewa na Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasilino Simba SC Ahmed Ally kwa kusema, Uongozi upo makini na unakamilisha baadhi ya taratibu za wachezaji waliopendekezwa na Benchi la Ufundi na muda si mrefu watatangazwa hadharani.

Ahmed amesema Mashabiki na Wanachama wa Simba SC wanatakiwa kuwa na imani na Uongozi wao, kwani wanatambua dhamira yao ya kuona timu inafanya vizuri, hivyo hawatafanya makosa katika usajili wa wachezaji watakaosajiliwa klabuni hapo katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo.

“Wana Simba watulie kwa kuwa tupo Chimbo , wasichanganywe na majina yanayotajwa hapa na pale, sisi tuna Road Map yetu ya usajili, tutafanya usajili mkubwa kuanzia eneo la Ushambuliaji.”

“Kwa kuwa bado hatujaridhishwa na magoli 5, 7 sasa tunataka magoli kuanzia 10 na kuendelea na pia tupo kwenye maboresho makubwa katika eneo letu la kiungo nadhani muda si Mrefu mtajulishwa” amesema Ahmed Ally

Simba SC tayari imeshakamilisha usajili wa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burundi Saido Ntibazonkiza, ambaye kwa mara ya kwanza alionekana akiwa na Jezi ya Klabu hiyo ya Msimbazi katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo uliopigwa Desemba 30-2022, ulishuhudia Kiungo huyo akifunga mabao matatu ‘Hat Trick’, huku Simba SC ikiibuka na ushindi wa mabao 7-1.

Chanzo: dar24.com