Mestalla, nyumbani kwa Valencia CF, ni uwanja wa zamani zaidi katika LALIGA na pia mojawapo ya viwanja vyenye mvuto zaidi.
Mazingira yenye shauku yanakwenda mbali hata kabla ya mechi, hasa kutokana na uamuzi wa Valencia CF wa kushirikiana na wasanii na ma DJ katika mechi zao za nyumbani.
Kwa hali inavyokwenda hapa nchini kwa mashabiki wa timu Fulani inayopitia magumu, suala hili lilikuwa zuri sana.
Valencia imefanya hivyo ili kutoa hamasa na burudani kwa mashabiki na kufanya biashara inayofanikiwa ndani ya jiji, Valencia CF ilifikia makubaliano na Palau Alameda, moja kati ya mtumbuizaji mkubwa huko Valencia.
DJs wa kudumu wa Palau Alameda watapiga muziki Mestalla saa moja na nusu kabla ya kuanza kwa kila mchezo wa nyumbani wa Valencia CF.
Vilevile, klabu ilimewaalika Elena Farga, mwimbaji kutoka Valencia, kutoa burudani kwenye uwanja waMestalla kabla ya mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Atlético de Madrid.
Mwanamuziki huyo amepata umaarufu hivi karibuni kwa kuwa mwandishi wa wimbo rasmi wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania katika Kombe la Dunia la Wanawake la FIFA 2023, ambalo La Roja walishinda.
Uamuzi wa Valencia CF wa kufanya kazi na wasanii wa ndani ili kuchangamsha sherehe za kabla ya mchezo ulichukuliwa kwa kuzingatia mashabiki.
Taasisi ya Valencia imejitolea kutoa burudani kwa mashabiki ambayo inakwenda mbali na mechi ya soka, na mashabiki wamejibu kwa njia chanya, wengi wao sasa wakichagua kufika mapema kabla ya kuanza kwa mchezo ili kufurahia mazingira haya. Zaidi ya hayo, klabu imetoa sababu ya kuwepo kwa wasanii waalikwa hawa:
“Kwa vitendo kama hivyo, kama lile la Farga, tunadhihirisha msaada wa klabu kwa wasanii wa ndani ambao wanashiriki maadili ya Mediteranea yanayoelezea namna yetu ya kuwa, kuungana, na kushiriki hisia, jambo ambalo pia ni msisitizo wa Valencia CF kwa msimu huu.”
Zaidi ya hayo, taasisi ya Valencia imeeleza jinsi wazo hili lilivyotokea, ikisema: “Wazo lilizuka kutokana na hamu ya kuimarisha uzoefu wa mashabiki katika mechi za soka ili kuzidi dakika 90 za mchezo, tulikuwa tunatafuta njia ya kuongeza burudani zaidi kabla ya mechi.
Mchanganyiko wa muziki na soka unachochea msisimko, bila shaka. Inawapa mashabiki uzoefu wa mchezo wenye utajiri zaidi na wa kumbukumbu.”
Mbali na kuboresha uzoefu wa mashabiki, aina hizi za maonyesho pia huchangia kuboresha mazingira na kufanya Mestalla kuwa uwanja mgumu zaidi kwa timu za wageni kutembelea.