Mashabiki wa Tottenham wamechukizwa na kitendo cha mabosi wa klabu hiyo kusuasua kufanya usajili katika dirisha dogo la usajili ambalo linafungwa usiku wa leo.
Mashabiki hao wameishambulia akaunti ya Instagram ya klabu hiyo kwa maneno makali huku wakimtuhumu Mwenyekiti wao Daniel Levy kwani yeye ni chanzo cha haya yote.
Hivi karibuni Tottenham ilikuwa ikinyemelea saini ya nyota anayecheza ligi isiyofahamika ya Isthminian Olli Tanner, lakini uhamisho huo ukakwama licha ya kufikia makubaliano ya maslahi na klabu yake ya Lewes.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 19 alikuwa akiwindwa na timu kibao za Ligi Kuu England zikiwemo Southampton, na Brighton.
Spurs imetangaza rasmi kuhusu dili hilo kwamba wamshindwa kufikia makubaliano na Lewes hivyo kinda huyo hatasajiliwa katika dirisha hili huku Lewes nao wakitoa ujumbe wa maneno kuhusu sakata hilo kupitia tovuti yao.
“Tunathibitisha kwamba hatujafikia makubaliano binafsi na klabu ya Tottenham kuhusu mchezaji wetu, hivyo Lewes atabaki kuwa mchezaji wetu,”
Hadi sasa Tottenham imekosa saini ya Adama Traore na Luis Diaz baada ya kuzidiwa kete na Barcelona na Liverpool.