Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki Tabora Utd waitaka Simba Ali Hassan Mwinyi

Tabora United Al Hassan Mwinyi Mashabiki Tabora Utd waitaka Simba Ali Hassan Mwinyi

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kufuatia kufungwa kwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi unaotumiwa na Tabora United katika Ligi Kuu Bara, mashabiki wa soka Manispaa ya Tabora wamewataka wahusika kuhakikisha uwanja huo unatimiza vigezo na kufunguliwa kabla ya mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Desemba 22

Wakizungumza mjini Tabora walisema walifurahi kupata timu ya Ligi Kuu, lakini kwa kufungiwa uwanja huo wanaona umuhimu wa kuwa na timu haupo.

"Tulifanya kadri ya uwezo wetu kuhakikisha tunapata timu Ligi Kuu sasa kwa kufungiwa uwanja tunakuwa tunapoteza maana," alisema Said Mohamed, huku Shukuru Ismail alisema wamiliki wa uwanja huo ambao ni CCM, lazima waurekebishe uwanja huo kabla ya mchezo huo na Mnyama, kwani wanatatka kuishuhidia 'live'.

Uongozi wa CCM kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi Mkoa wa Tabora, Idd Moshi Mambo aliwapoza mashabiki wa soka akisema jitihada zinafanyika kuurekebisha uwanja huo sehemu za mitaro na kwamba michezo ya ligi kuu ya NBC itaendelea kuchezwa kwenye uwanja huo

"Marekebisho ni kwenye mitaro jambo haliwezi kutumbua kwani tutarekebisha mara moja na uwsnja kuendelea kutumika," alisema

Aliwataka mashabiki wa soka kutokuwa na wasiwasi kwani kasoro zilizoelezwa sio kubwa sana kama walivyokuwa wanadhani na kwamba mchezo wa Ligi Kuu unaosubiriwa kwa shauku kubwa dhidi ya Simba akisisitiza utapigwa hapo hapo Ali Hassan Mwinyi.

Kwa upande wa Msemaji wa Tabora United, Pendo Lema akizungumza kutoka mkoani Mbeya, alisema kwa sasa timu hiyo itautumia Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma wakati Ali Hassan Mwinyi unafanyiwa marekebisho katika mchezo wa Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Monduli Coffee ya Lindi itakayopigwa Desemab 16.

Tabora iliyopanda Ligi Kuu msimu huu kutoka Ligi ya Championship kesho Ijumaa itakuwa ugenini kuvaana na Ihefu kwenye mchezo utakaopigwa Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya.

Chanzo: Mwanaspoti