Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki TP Mazembe kuandamana

Tp Mazembe Fans.jpeg Mashabiki TP Mazembe kuandamana

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa kutoka kwa Mwandishi wa habari wabkujitegemea kutoka Goma Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Richard Muhima, inaeleza kua huwenda mashabiki wa TP Mazembe wakaandamana siku yoyoyte.

Hii kufuatia Serikali ya Nchi hiyo kushindwa kutoa kibali Cha kuruhusu kuingizwa Kwa vifaa vya kurushia Matangazo ya Television ya mchezo wa African Football League dhidi ya Esperance.

Jambo hili linaonekana kua ni la kisiasa zaidi, Kwani Mmiliki wa timu hiyo ya Lubumbashi Moise Katumbi Chapwe ni mmoja ya watakaosimama kuwania kitu Cha Urais wa Nchi katika uchaguzi ujao.

Na inaaminika nyuma yake kuna Watu wengi wanaomuunga mkono, Hivyo kitendo cha Serikali kutotoa idhini ya vifaa hivyo inatafsirika kama Fitna ya kumpinga Katumbi katika kuinyima nafasi Mazembe ya kuonekana.

Ikiwa zimesalia siku 6 kuelekea mchezo huo, kama mambo yatakua magumu basi Huwenda TP Mazembe wakachagua Uwanja wa Benjamin Mkapa wa Dar kwa ajili ya mchezo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live