Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki Moro wajadili kauli za Hayati JPM kwenye michezo

Moro Pic Data.png Mashabiki Moro wajadili kauli za Hayati JPM kwenye michezo

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wadau na wapenzi wa soka Manispaa ya Morogoro wamechambua kauli za kimichezo zilizowahi kutolewa na aliyekuwa Rais wa Tano wa Tanzania , Dk John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17 mwaka huu jijijni Dar es Salaam kuwa zimeifaidisha Simba SC katika michezo ya kimataifa.

Moja ya kauri hizo ni ile ya Mei 19 ambayo Simba SC ilikubali kipigo cha bao 1-0 na Kagera Sugar Uwanja wa Mkapa na kusema kuwa timu hiyo imetobolewa tundu moja akiwa na maana imepoteza mchezo wa mwisho wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 kabla kuwakabidhi kombe la ubingwa huo.

Wakizungumza na Mwandishi wa gazeti hili mkoani hapa, wadau hao walisema kuwa kauri za Dk Magufuli zilikuwa zinawaamsha viongozi katika usingizi wa kuongeza maarifa, tija na ubunifu kwa ajili ya maendeleo ya soka katika ngazi ya vilabu na timu za taifa kwani unapokosolewa ndio unajifunza.

Upendo Mizambwa alisema kuwa anayekosoa jambo anakupa nafasi ya wewe kujifunza wapi umeteleza na kufanya masahihisho yanayopelekea kufanya vizuri jambo lako siku nyingine.

“Mimi ni mshabiki wa Simba SC na moja ya kauri ambazo nimeweza kuzitafakari ni ile iliyotolewa na Dk Magufuli ya kuwa klabu yake ya imetobolewa tundu moja ilikuwa na maana Simba imepoteza mchezo mbele ya Kagera Sugar,” alisema Mizambwa.

Mizambwa alisema kuwa kauri ya kutobolewa tundu moja imekaa kimchezo zaidi lakini viongozi, wachezaji na wadau wa klabu, siku ile hawakuwa na furaha kwanza baada ya kupoteza mchezo tena mbele ya rais licha ya kukabidhiwa kombe yeye alikuwa na furaha nusu.

“Huyu baba (Dk Magufuli) kifo chake kimeniumizaa sana lakini kauri zake zitafanyiwa kazi zaidi na wanamichezo endapo watataka kubadilika kiongozi na wachezaji kujitambua katika michezo ili kuiletea maendelea klabu zao na timu za taifa za Tanzania," alisema Mizambwa.

Mizambwa alisema kuwa hapendi michezo isipokuwa amekuwa akifurahia Simba SC inapofanya vizuri na binafs timu hiyo ikipoteza mchezo hukosa furaha.

Mwanachama wa Simba SC, Nasoor Chamchua alisema kuwa klabu hiyo inaishi na maneno ya Magufuli na klabu hiyo imekuwa chachu ya kufanya vizuri ligi ya ndani na ligi ya mabingwa afrika lakini kifo cha Dk Magufuli kimetoa funzo kwa kauri zake katika michezo.

Chamchua alisema kuwa mwaka huo 2018 uongozi wa klabu yao iliendelea kufanya maboresha katika benchi la ufundi na kusajili wachezaji wenye uwezo wa kuipigania katika michezo ya ligi ya ndani na nje.

“Kifo cha Rais Magufuli kimetibua mambo mengi katika michezo hasa pande wa klabu ya Simba, nilitamani siku mmoja Magufuli ashuhudie simba ikifika mbali ligi ya mabingwa wa afrika tofauti ya miaka ya nyuma," alisema Chamchua.

Chamchua alisema kuwa ligi ya mabingwa wameshuhudia Simba SC ikifanya vibaya kwa kufungwa bao 5-0 lakini kadili siku zilivyokuwa zinaenda uongozi uliendelea kuimarisha timu na sasa wanafanya vizuri ligi ya mabingwa na ligi ya ndani hivyo hali ikiendelea hivyo huenda wakatwaa ubingwa huo wa kombe la afrika mwaka huu.

Kwa upande wa shabiki wa klabu ya Yanga SC, Lazaro Ambrose alisema anatamani Rais Samia Hassan Suluhu afuate nyayo zake za kuipata sapoti timu za taifa za vijana na wakubwa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz