Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki Azam, Coastal mdogo mdogo

Mdogo Mdogo Mashabiki Azam, Coastal mdogo mdogo

Thu, 8 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki mbalimbali wameendelea kujitokeza mdogo mdogo kwa ajili ya kununua tiketi za mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii, kati ya Azam FC dhidi ya Coastal Union utakaopigwa saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

Mwanaspoti ambalo limewe kambi visiwani hapa kwa ajili ya mchezo huo, limeshuhudia mashabiki wakiendelea kujitokeza kwa mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wadau wa soka.

Shabiki wa Azam, Ayoub Said ambaye ametoka jijini Dar es Salaam hadi Zanzibar ili kushuhudia mchezo huo, amesema hana wasiwazi na wapinzani wao Coastal, huku akitamba mechi ya leo ni sehemu tu ya maandalizi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Azam tuna timu nzuri na leo tutawaonyesha Coastal Union kwamba sisi wachezaji wetu ni bora kuliko wao, hivyo wasitarajie mteremko kabisa," amesema Ayoub na kuongeza;

"Sina maana naidharau Coastal Union isipokuwa ubora wa wachezaji ambao Azam FC inao ndio unaonifanya kuamini tunaweza kutinga fainali ya Ngao ya Jamii na kuchukua ubingwa."

Kwa upande wa Ally Masoud aliyejitambulisha shabiki wa Coastal Union amesema, Azam kitakachoiponza ni kuwadharau na kuona wana kikosi imara hivyo wategemee mchezo mgumu uwanjani tofauti na matarajio yao.

Timu hizo zinakutana katika mchezo huo wa mapema kabla ya hapo jioni miamba wa soka nchini Yanga na Simba kumenyana kuanzia saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Washindi wa mechi hizo za Dar na Zanzibar watavaana katika fainali itakayopigwa Jumapili, wakati zilizopoteza zitaumana kuwania nafasi ya tatu, michezo yote ikipigwa siku hiyo Kwa Mkapa.

Chanzo: Mwanaspoti