Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki Arsenal wamvaa Arteta kisa Bukayo Saka

Bukayo Saka New Season Bukayo Saka

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wa Arsenal wamemjia juu kocha Mikel Arteta baada ya kumchezesha Bukayo Saka katika mechi ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Lens wakati alikuwa ni majeruhi.

Kocha huyo aliweka wazi hali ya Saka baada ya kutolewa nje wakati mechi ikiendelea Arsenal ikipokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Lens. Lakini mashabiki wao walichukizwa kwani winga huyo hakuwa fiti kwa asilimia 100.

Arsenal itacheza dhidi ya Manchester City wikiendi hii lakini huenda Saka akakosa mchezo huo wa Ligi Kuu England kutokana na majeraha.

Saka alikuwa chini akiugulia jeraha lake kwa muda mrefu wakati wa mechi dhidi ya Lens kabla ya kufanyiwa mabadiliko nafasi yake ikichukuliwa na Fabio Vieira katika dakika ya 33.

Sasa mashabiki walishindwa kujizuia wakimtupia lawama Arteta kwani winga huyo alikuwa ana jeraha ambalo linamsumbua kabla ya mechi hiyo ya Ligi Mabingwa Ulaya. Kundi la Mashabiki wa Arsenal The Gooners wakaandika kupitia kupitia mtandao wa kijamii wa X wakidai: “Saka aliumia, Arteta alishindwa kumlinda vizuri. Kazi nzuri Arteta, umemchezesha Saka wakati ni majeruhi sasa tutamkosa kwa muda mrefu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live