Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki Arsenal wamkataa Kai Havertz

Kai Havertz Arsenal Kai Havertz

Sun, 1 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Mashabiki wa Klabu ya Arsenal wamemshinikiza Kocha wao, Mikel Arteta ampange Emile Smith Rowe badala ya Kai Havertz kufuatia kiungo kuonyesha kiwango bora kwenye mechi ya Kombe la Carabao dhidi ya Brentford.

Smith Rowe alianza kikosi cha kwanza kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Brentford na kuwapagawisha mashabiki wa Arsenal.

Shabiki mmoja aliandika kupitia akaunti ya X: “Rowe ni mchezaji mzuri kutokea Arsenal. Ni zaidi ya Havertz katika nafasi yake anayocheza.”

Mwingine aliandika: “Rowe anatakiwa kuanza kikosi cha kwanza. Tumechoka kumuona Havertz. Emily Smith alizaliwa kucheza nafasi hiyo (namba 8), hata anavyokimbia poa anashikiriana vizuri na Declan Rice utaona tu kuna kitu.”

Lakini mashabiki wa Arsenal walisikitika baada ya Arteta kuweka wazi kwamba mchezaji huyo bado sio fiti kwa asilimia 100 ameanza kurejea taratibu baada ya kupona majeraha aliyopata msimu uliopita.

Licha ya kuonyesha kiwango safi dhidi ya Brentford ambapo alifikisha mechi ya l0 akiwa na uzi wa Arsneal alifanyiwa mabadiliko dakika ya 68.

Arteta alisema: “Kimwili, hayupo vizuri, mkae mkijua tuna wachezaji watano wanaocheza nafasi moja, Rowe aliumia lakini hiyo sio sababu, tulimpangia dakika za kucheza, ilikuwa ngumu kuendelea na mechi sambamba na Reiss Nelson.”

Chanzo: Dar24