Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki 160 wakamatwa, polisi 103 wajeruhiwa Morocco

Farfes.jpeg Mashabiki 160 wakamatwa, polisi 103 wajeruhiwa Morocco

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Takriban mashabiki 160, baadhi wakiwa na visu na mawe, wamekamatwa katika mechi ya soka nchini Morocco jana Jumapili)katika vurugu zilizosababisha maofisa wapatao 100 wa polisi kuumia, viongozi wamesema.

Mashabiki hao, miongoni mwao wakiwa watoto 90, "walikamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika vurugu, kumiliki visu, ulevi, kurusha mawe, kusababisha uharibifu na kuchoma moto magari," imesema ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa (DGSN) katika taarifa yake.

Vurugu hizo ziliibuka mwishoni mwa mechi ya Kombe la Mfalme kati ya AS FAR, timu ya jeshi la Morocco ya jijini Rabat, na Maghreb de Fez (MAS).

AS FAR ilikuwa imefungwa mabao 2-0 na mashabiki wake wakavamia uwanja kukabiliana na wapinzani wao, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari. Polisi walirushiwa fataki wakati wakiingilia vurugu hizo.

DGSN iliripoti kuwa polisi 103 walijeruhiwa, wakati mashabiki 57 pia waliumizwa.

"Kwa hatua hii ya uchunguzi, tumeona uharibifu mkubwa katika uwanja wa Moulay-Abdallah. Pikipiki ilichomwa moto na magari 33 ya polisi na watu binafsi pia yaliharibiwa," imeongeza DGSN.

Shirikisho la Soka la Morocco litakutana wiki ijayo kujadili vurugu hizo na adhabu zinatarajiwa kutolewa.

Mlipuko wa vurugu hizo za Jumapili ni wa kwanza tangu mashabiki waruhusiwe kurejea viwanja mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya kuzuiwa kwa miaka miwili kutokana na ugonjwa wa Virusi vya Corona, Covid-19.

Hata hivyo, viwanja vya Morocco vimekuwa majukwaa ya vurugu za mashabiki katika miaka ya karibuni.

Mapigano hutokea mara kwa mara kati ya mashabiki wa klabu kubwa mbili za Casablanca, Wydad na Raja, ikiwa ni pamoja na katika mitaa nje ya viwanja.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz