Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maseke alikumbuka lile bao la Hafiz Konkoni

Hafiz Konkoni X Maseke Maseke alikumbuka lile bao la Hafiz Konkoni

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa wa KMC aliyesimama langoni na kuruhusu mabao 5-0, Wilbol Maseke amelikumbuka bao la straika mrefu wa Yanga aliyemtungua la tatu, Hafiz Konkoni na kummwagia sifa mwamuzi Omar Mdoe kumshtukia janja yake ya kutoa mpira ukiwa umevuka mstari.

Maseke aliyetua KMC baada ya kutemwa na Azam aliyokuwa akiichezea, alisema Mdoe anastahili kupewa maua kwa kazi aliyoifanya kwani angekuwa mwamuzi mwingine na kutokuwepo kwa VAR Yanga ingenyimwa bao hilo lililofungwa dakika ya 76 baada ya piga nikupige langoni mwake.

Kipa huyo alisema sio kila mara waamuzi walaumiwe tu, pale wanapotenda haki ni lazima wapewe moyo kama alivyofanya Mdoe kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga.

“Dakika 90 za mchezo kila mchezaji anakuwepo uwanjani kwa ajili ya kuitetea timu yake, nisingeweza kuuacha mpira uende kirahisi, kwani nami ulinibabatiza mikononi, ila ni kweli lilikuwa bao nilidaka nikiwa nimevuka mstari, ila nisingekubali kirahisi. Mwamuzi alikuwa makini na kutenda haki, kwa kweli anastahili pongezi na hii iendelee isiwe kwa KMC iwe kwa timu zote,” alisema Maseke.

“Ni kweli nimefungwa mabao 5-0 katika hayo labda la Mudathir Yahya ndilo naweza kulisifu kwani alilipambania na lilikuwa la kiufundi zaidi, mengine ya kawaida sana, likiwamo hilo la Konkoni.”

Akimuelezea Mudathir alisema alimuona ni mchezaji aliyehusika na mipira mingi zaidi ya hatari upande wao na anaamini kwamba ndiye alikuwa nyota wa mchezo huo (man of the match).

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: