Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masau Bwire anusurika kifo Dar

Masau Bwire Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire

Thu, 3 Mar 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MSEMAJI wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amepata ajali maeneo ya Buguruni jijini Dar es Salaam leo Machi 3 mchana akiwa na gari yake aina ya Toyota Rav 4.

Akizungumza Bwire amesema, ajali hiyo imetokea mchana huu akiwa njiani kuelekea Mzizima.

''Nilikuwa natokea Ilala Boma nafika Buguruni nakutana na shida hiyo kusema ukweli huyo jamaa amenigonga, ila niko salama,'' anasema Bwire.

"Daladala imetaka kunipita basi nikamtizama kwenye kioo akaja akanivaa, sema gari ni ngumu ingekuwa gari nyepesi ingeharibika sana,"

Anasema kwa mbele na nyuma ya gari yake ndipo palipopata shida sana.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz