Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masau Bwire afunguka kumrithi Manara Simba

MASAU BWIRE 11 Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire

Sun, 12 Sep 2021 Chanzo: salehejembe.blogspot.com

Wakati tetesi zikieleza kuwa muda wowote Ofisa Habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire atakabidhiwa mikoba ya Haji Manara, kiongozi huyo ameweka wazi kuwa kila kitu kitakuwa wazi hivi karibuni.

Ni Kaimu Ofisa Habari, Ezekiel Kwamwaga kwa sasa anashikilia kwa muda nafasi hiyo baada ya kupewa mikoba kwa muda wa miezi miwili na alibainisha kwamba ataondoka katika nafasi hiyo.

Akizungumzia tetesi hizo, Masau Bwire ambaye wengi hupenda kumuita mzee wa kupapasa amesema

”Hizo za kuhusu mimi kwenda Simba ni tetesi zipo kila kona, siku ikifika watu watajua pale wenye mamlaka watakaposema.

“Unajua mimi ni mzalendo si kwa Simba tu hata kwa Yanga nimefanya sana kutoa hamasa hasa kwenye masuala yanahohusu taifa. Mimi nina kawaida ya kuhamasisha pale timu inapokuwa na jambo linaloihusu Tanzania kwa kuwa ninajua hiyo ni fursa".

“Najua haya yametokana na watu kuona mimi nikizungumzia kuhusu Simba lakini hii Simba day kuna watu wanafuatilia nje ya Tanzania, wakiona kuna nyomi, watu wanaona kuna kitu kinaendelea, tushirikiane Watanzania tuache roho ya korosho".

“Kwa mfano tarehe 25/11-15/12 kutakuwa na mashindano ya soka la wenye ulemavu na Tanzania itakuwa mwenyeji, mpaka wakupe fursa hiyo ni watu wamekuamini na mimi nitakuwa msemaji rasmi kwenye mashindano hayo makubwa yatahusisha timu 16 na wanatafuta timu 8 zitakazoshiriki mashindano Uturuki hivyo Watanzania tuungane,” amesema Bwire.

Chanzo: salehejembe.blogspot.com