Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masau Bwire: Tuombeeni Ruvu Shooting

Masau Kuliga Bwire 1 1?fit=800%2C574&ssl=1 Masau Bwire: Tuombeeni Ruvu Shooting

Fri, 5 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, amesema kwa hali waliyonayo kwa sasa kwenye msimamo wa Ligi Kuu, ni maombi kwa Mungu tu ndiyo yanaweza kufasaidia kubaki Ligi Kuu ya NBC.

Ruvu kwa sasa wapo mkiani kabisa kwenye msimamo wakiwa na alama 20 huku mkononi wakiwa wamebakiwa na mechi tatu pekee za kuweza kujitetea kama wanatoka mkiani au la.

"Tuna mechi tatu pekee tumebaki nazo mkononi na hizo mechi kwa sasa tuna Simba SC, Singida Big Stars na Dodoma. Ukiangalia hapo kwa kweli kwa kuanza tutacheza na Simba na umeona ubora wao kwenye mechi za Kimataifa hata kama wametolewa lakini ubora wao tumeuona.

"Ndio maana ninasema kwa kweli mtuombee, Watanzania wenye mapenzi mema na Ruvu tunaomba sana mtuombee tubaki Ligi Kuu, tuwaombee wachezaji wa Simba wakifika golini kwetu wapate mchecheto wasifunge na sisi tukifika kwao tufunge," alisema Masau.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live