Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masau Bwire: Hatushuki daraja

SAU BWIRE Masau Bwire: Hatushuki daraja

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, amesema wanaziangalia mechi zao nne zilizosalia kwenye Ligi Kuu ya NBC kwa jicho la tofauti ili waweze kujinasua nafasi ya pili kutoka mkiani kwenye msimamo.

Masau ameyazungumza hayo wakiwa kwenye maandalizi wa mchezo wao wa kwanza kati minne iliyobaki dhidi ya Azam FC mchezo utakaochezwa kesho Aprili 22, 2023.

"Tunaingalia hii michezo yetu kwa namna tofauti sana kuliko watu wanavyofikiri kwamba tunashuka daraja, sisi tutacheza vizuri ili kujitoa huku kwenye nafasi ya hatari tulipo," alisema Masau.

Michezo iliyosalia kwa Ruvu mbali na Azam, watakipiga na Simba SC, Dodoma Jiji na Singida Big Stars.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live