Kipa wa Ihefu, Hussein Masalanga ‘Buffon’ amesema maisha ni mazuri ndani klabu yake hiyo mpya huku akiahidi mambo mazuri zaidi.
Masalanga amejiunga kwa mkopo na Ihefu akitokea Ruvu Shooting ya mkoani Pwani aliyoitumikia mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.
Kipa huyo akiwa Ruvu alianza katika michezo yote ya mzunguko wa kwanza akidaka kwa dakika 1440.
Masalanga ambaye msimu uliopita aliidakia Dodoma Jiji alisema baada ya kufanya vizuri na Ruvu ameona atafute changamoto mpya na Ihefu ni sehemu sahihi.
Nyanda huyo alisema maisha ya Ihefu ni mazuri na ana imani ataonesha uwezo wake na kuisaidia timu hiyo katika michezo ya Ligi Kuu Bara.
“Kambi ni nzuri maisha ni mazuri sasa ni kupambana ili kuonesha kitu ambacho ninacho nashukuru nimepokelewa vizuri,” alisema kipa huyo chipukizi katika Ligi Kuu Bara.