Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masaa matano mazito Yanga

Mexime Yanga Pic Data Masaa matano mazito Yanga

Fri, 19 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Khatimu NahekaMore by this Author ACHANA na tukio la Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla kutolewa maneno machafu na mashabiki baada ya kumalizika kwa sare ya mabao 3-3 na Kagera Sugar.

Mechi ilipoisha tu, vigogo wote unaowajua wa Yanga waliwasha magari yao na kulifuata nyuma basi la wachezaji mpaka kambini - Kigamboni, huku wachezaji wakijua kwamba ni ishu ya kawaida tu na yataisha goma likageuka.

Iko hivi; walipofika kambini tu wachezaji walipitiliza vyumbani kuoga na baadaye kula.

Lakini kwenye mida ya saa tano wakiwa wanajiandaa kwenda kulala mara paap! Akaibuka Meneja Hafidh Saleh na kutoa ujumbe kwa kapteni Lamine Moro kwamba wachezaji wote wanatakiwa kwenye ukumbi wa mikutano. Makocha wakaambiwa wasubiri kidogo nje.

Walipoingia ukumbini wakakutana na vigogo kibao wa Yanga wakiongozwa na Msolla, Hersi Said ambaye ni makamu mwenyekiti wa Kamati ya Usajili pamoja na Senzo Mazingisa ambaye ni mshauri wa Yanga kwenye mabadiliko. Baada ya Salamu wakaulizwa tatizo ni nini, mbona timu inayumba?

Wakiwa wanajiandaa kujibu wakasisitizwa kwamba wawe wawazi kwani kikao hicho kitakuwa ni siri kubwa baina yao na viongozi na kila kitu kitaishia ndani - hapo, lengo likiwa ni kujenga na kurudi kwenye ramani ya ushindi.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz