Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Marufuku kupiga mpira kichwa'

96961 Pic+kichwa 'Marufuku kupiga mpira kichwa'

Wed, 26 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Viongozi wa soka wa England, Scotland na Ireland Kaskazini wametangaza kupiga marufuku kupiga mpira kichwa mazoezini kwa watoto hadi watakapomaliza elimu ya msingi, na marufuku hiyo inaanza mara moja. Vyam,a hivyo vitatu vya soka vilitoa taarifa ya kuthibitisha mabadiliko katika muongoza wa upigaji mpira kichwa, ambao unatokana na utafiti ambao unaonyesha uwezekano wa wanasoka wa zamani kufariki kwa magonjwa yatokanayo na nyurolojia mara tatu zaidi ya watu wengine. Mabadiliko hayo yanaeleza kuwa hakutakuwa na upigaji mpira kichwa kabisa katika "ngazi ya msingi"-- kwa watoto wa shule za msingi -- na watakaovuka wataweza kupiga mpira kichwa katika mazoezi ya watoto walio na umri kati ya miaka 12 na 16. Hakutakuwa na mabadiliko ya kupiga mpira kichwa katika mechi, kwa kuzingatia kuwa hutokea mara chache. Utafiti huo, ulioongozwa na Chuo Kikuu cha Glasgow, haukueleza kwamba upigaji mpira kichwa ni chanzo cha kuwepo kwa ongezeko la tatizo la nyurolojia miongoni mwa wanasoka, lakini uamuzi wa kubadilisha mwongozo umechukuliwa kwa lengo la kukabiliana na uwezekano wowote wa hatari, chama cha soka chas Uingereza, FA kimesema. Mtendaji mkuu wa FA, Mark Bullingham alisema: "Mabadiliko haya ya mwongozo wa upigaji kichwa mpira ni mwendelezo wa mwongozo wa sasa na utasaidia makocha na walimu kupunguza na kuondoa upigaji kichwa unaojirudiarudia na usio na umuhimu katika soka. "Utafiti wetu umeonyesha ni nadra sana kunakuwa na upigaji kichwa mpira katika mechi za soka za vijana, kw ahiyo mwongozo huu ni maendeleo muhimu katika ufundishaji wa soka la watoto bila ya kuathiri burudani ambayo watoto wa umri tofauti hupata kwa kucheza soka." Vyama hivyo vimesema mwongozo huo umetolewa sambamba na kamati ya afya ya Chama cha Soka cha Ulaya (Uefa), ambacho kinataka kutoa mwongozo wa bara zima baadaye mwaka huu.

Chanzo: mwananchi.co.tz