BEKI wa Manchester United Lisandro Martinez atakuwa nje ya dimba kwa muda wa miezi mitatu kutokana na jeraha la mguu kwa mujibu wa taarifa.
Inaaminika kwamba beki huyo wa kimataifa wa Argentina alifanyiwa upasuaji wa mguu wake wa kulia ambao ulikuwa unampa shida.
Muargentina huyo, 25, alikumbana na jeraha la mguu kwa mara ya kwanza Aprili mwaka huu na alikuwa nje kwa wiki 11. Beki uyo alirejea wakati wa maandalizi ya msimu mpya na aliichezea Man Utd mechi nne za ufunguzi za Ligi Kuu England.
Lakini beki huyo alijitonesha tena wakati wa mechi dhidi ya Arsenal ambayo ilipokea kichapo cha mabao 3-1 mwezi uliopita na akatolewa nje.
Madaktari wa Man United walimpa huduma ya kwanza ya kutulia maumivu ili kupunguza makali kufuatia kichapo dhidi ya mabao 3-1 dhidi ya Brighton na Bayern Munich.
Lakini vipimo vyake vilivyotoka wiki hii vinaonyesha kwamba beki huyo bado hajapona vizuri na kuna uwezekano wa kufanyiwa upasuaji haraka iwezekanvyo ili kutibu jeraha.
Na beki huyo wa kati wa Argentina alikuwa akijiandaa kufanyiwa upasuaji kwenye mguu wake wa kulia ili kujaribu kutibu tatizo lake la muda mrefu.
Hivyo inaweza kumweka nje kwa hadi miezi mitatu ikimaanisha kuwa anaweza asirudi hadi mwakani.Akizungumzia juhusu jeraha hilo wiki iliyopita Erik ten Hag alisema: "Tulifanya uchunguzi vizuri hata alipokuwa huko Argentina, lakini sasa tatizo limeibainika. Inasikitisha sana, kwake na kwa timu."
Kutokana na kutokuwepo Martinez, Raphael Varane, Victor Lindelof, Jonny Evans na Harry Maguire ndio machaguo ya mabeki wa Ten Hag waliobaki kwa sasa.