Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Martinez hajakata tamaa na Hazard, amjumuisha kikosini

Eden Hazard Called Up Eden Hazard

Fri, 11 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha timu ya taifa cha Ubelgiji kimetangazwa mchana wa leo kitakachokwenda nchini Qatar kwwajili ya kushiriki michuano ya kombe la dunia huku nyota wa Real Madrid Eden Hazard akiendelea kuwepo kwenye kikosi hichi chini ya mwalimu Roberto Martinez raia wa Hispania.

Licha ya kutokupata nafasi ya kucheza mara kwa mara ndani ya kikosi cha Real Madrid lakini kocha wa timu hiyo amemuita nyota huyo wa zamani wa klabu ya Chelsea.

Eden Hazard amekua akisumbuliwa na majeruhi mara kwa mara tangu ajiunge katika klabu ya Real Madrid mwaka 2018 jambo ambalo limefanya nyota huyo kutopata nafasi ya kucheza zaidi kwenye kikosi cha Real Madrid.

Licha ya kutokupata nafasi ndani ya Real Madrid Hazard amekua akicheza kwa kiwango cha hali ya juu anapoitwa kwenye timu ya taifa, Hivo nyota huyo ameendelea kua mwanajeshi mtiifu wa kocha Roberto Martinez.

Pia nyota wa klabu ya Intermilan Romelu Lukaku amejumuishwa kwenye kikosi hicho licha ya kutoka kwenye majeruhi siku kadhaa zilizopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live