Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Martinez asema yeye ni kama Mbappe

Lautaro Martinez Mahakama Lautaro Martinez

Mon, 27 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Inter Milan, Lautaro Martinez anaamini yuko kwenye levo sawa na Kylian Mbappe, Erling HaalandA, Harry Kane na Robert Lewandowski.

Martinez ambaye amekuwa akihusishwa na timu mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Manchester United na Arsenal, alichukua tuzo ya mfungaji bora wa Serie A msimu uliopia akimaliza na mabao 24.

Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2026 lakini kuna tetesi huenda akauzwa dirisha hili na PSG pia inamwangalia kama mbadala wa Mbappe.

Katika mahojiano na La Gazzetta dello Sport, Martinez aliulizwa ikiwa anaamini yeye ni kati ya washambuliaji bora zaidi ulimwenguni kama Mbappe, Haaland, Kane na Lewandowski, alisema sina chuki nao lakini namba na vikombe vinaongea.

“Baadhi yao wameshinda kidogo kuliko mimi. Ni lazima niendelee kufanya kazi kwa kuwajibika kama baba yangu alivyonifundisha, lakini naamini huenda nipo katika kiwango sawa na wachezaji hao wakubwa.”

Kumekuwa na ripoti kutoka Italia zinazodai Inter na Martinez hawajafikia mwafaka wa mkataba mpya kutokana na masuala la mishahara, mchezaji anataka Euro 14 milioni kwa mwaka wakati Inter inataka kumpa Euro 8 milioni kwa mwaka.

Wakala wake alipoulizwa juu ya uwezekano wa Lautaro kuondoka ama kubaki alisema bado mazungumzo yanaendelea hivyo hahitaji kuweka wazi kila kitu.

Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2026 lakini kuna tetesi huenda akauzwa dirisha hili na PSG pia inamwangalia kama mbadala wa Mbappe.

Chanzo: Mwanaspoti