Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Martinez afichua alichomwambia Romero Fainali Kombe la Dunia

Emiliano Mrtinez X Romero Martinez afichua alichomwambia Romero Fainali Kombe la Dunia

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waswahili waliwahi kusema "Usione Vyaelea Vimeundwa". Nyuma ya Mafanikio kuna Jitihada nyingi na umakini mkubwa unafuatwa.

Hapa Golikipa wa Argentina Emiliano Martinez anatusanua namna ambavyo yeye binafsi alipambana kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Ufaransa

"Nililazimika kumwambia beki wangu Cristian Romero mara kwa mara aache kufanya Tackling ngumu, aache kabisa kwasababu zinaweza kutugharimu. Katika mechi ile ya fainali, nilikuwa namwambia kabla ya mechi, wakati wa mechi na hata muda mapumziko. Kwa msisitizo zaidi nilikuwa namwambia, leo ukipata kadi nyekundu ujue kabisa baada ya mechi nakupiga kama sikufahamu"

Hii ilikuwa ni zaidi ya kivumbi na jasho, ukichoma unalo

Romero alimaliza mechi bila kuonyeshwa kadi yoyote, na ndiye beki aliyemaliza na Rate kubwa zaidi (4.0) kwa timu zote mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live