Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Martinez: Messi anatupa ari ya ushindi

B497733D 6DB3 48E3 992B 99CA84719397.jpeg Mlinda mlango wa Argentina, Emiliano Martinez anaamini Messi ndio chachu ya ushindi wao

Sun, 18 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Golikipa wa timu ya taifa ya Argentina, Emiliano Martinez amesema kua nahodha wa timu hiyo Lionel Messi anawapa faida zaidi ya kushinda mchezo wa fainali dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa.

Lionel Messi atacheza mchezo wa fainali wa jumapili dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa na atakua anaweka rekodi kama mchezaji aliecheza michezo mingi kwenye michuano hiyo akiwa amefikisha michezo 26.

Lionel Messi amekua kwenye kiwango bora sana kwenye michuano ya kombe la dunia baada ya kuisaidia timu yake kutinga fainali ya michuano hiyo, Huku akiwa anaongoza kua mchezaji mwenye mchango mkubwa wa mabao akiwa amefunga mabao matatu na kupiga pasi tatu za mabao hiivo mchango wake ni mabao 8.

Kipa Martinez anasema kuwepo kwa Messi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kunawapa nguvu wachezaji wote wa kikosi hichi kwasababu wana mchezaji bora duniani kwenye kikosi chao kitu ambacho kinawapa faida.

Emiliano Martinez ambaye amekua kwenye ubora mkubwa kwenye michuano hii amesema anajua watu wengi watawapa nafasi zaidi timu ya taifa ya Ufaransa, Lakini wao wana mchezaji anaeweza kufanya vitu vya ziada na kuwapa faida zaidi wao ambaye si mwingine ni Lionel Messi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live