Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Martinelli apiga mbili, Arsenal yaua 4-1

Gabriel Martinelli 030c243 Gabriel Martinelli, alifunga magoli mawili usiku wa jana

Sun, 19 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Leeds United wamechapwa mabao 4-1 na Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Elland Road mjini Leeds, West Yorkshire.

Mabao ya Arsenal yamefungwa na Gabriel Martinelli mawili dakika ya 16 na 28, Bukayo Saka dakika ya 42 na Emile Smith Rowe dakika ya 84, wakati la Leeds United limefungwa na Raphinha kwa penalti dakika ya 75.

Arsenal inafikisha pointi 32 baada ya ushindi huo na kujiweka sawa nafasi ya nne, wakati Leeds United inabaki na pointi zake 16 katika nafasi ya 16 baada ya wote kucheza mechi 18.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live