Wakala wa mchezaji wa Manchester United, Anthony Martial amesema mteja wake amewasilisha rasmi ombi la kuomba kuondoka ndani ya klabu hiyo katika majira ya baridi.
Martial, 26 amefanikiwa kucheza mechi mbili pekee za Ligi kuu ya EPL msimu huu akiwa amefunga bao moja kutokana na majeraha na kiwango chake kushuka mara kadhaa.
“Martial angependa kuondoka United mwezi January. Anachotamani ni fursa ya kucheza na asingependa kuwepo Manchester msimu ujao. Nitazungumza na waajiri wake kuhusu hatma yake, ” alisema wakala wake, Philippe Lamboley
Meneja mpya wa Man United, Raph Rangnick aliweka wazi mpango wa kutaka kuwaachia kwa mkopo wachezaji kadhaa kwa mkopo mwezi January kutokana na kukosa nafasi ya kucheza.