Mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial amemwambia kocha wake Ralf Rangnick anahitaji kuondoka ndani ya klabu hiyo kutafuta changamoto mpya mahala pengine.
Martial, 26 anahitaji kuondoka katika dirisha la usajili la mwezi Januari kwaajili ya kupata nafasi ya kucheza zaidi katika kikosi cha kwanza na kocha wake amethibitisha hilo.
Wiki chache zilizopita wakala wa mchezaji huyo pia alidhibitisha kuhusu mteja wake kutaka kuondoka Old Trafford na sasa meneja Ralf Rangnick ameweka wazi kuhusu azma ya mchezaji huyo.
“Tumeongea kwa kirefu. Amenielezea amekuwepo Manchester United kwa kipindi cha miaka saba sasa na anadhani ni muda sahihi kufanya mabadiliko, kwenda mahali pengine” alisema Rangnick.
“Hakuna ofa yoyote mpaka sasa kwake, endapo kuna ofa tutaangalia lipi bora kwa mchezaji na klabu, tofauti na hapo ataendelea kusalia klabuni.” aliongeza.