Beki wa kimataifa wa Brazil ambaye ni nahodha wa klabu ya PSG Marquinhos amekaribia kusaini mkataba mpya na wababe hao wa soka la Ufaransa wa kuendelea kusalia kwenye viunga vya Parc de Princes.
Beki Marquinhos inaelezwa kwa sasa ana asilimia 100 ya kuendelea kuwatumikia mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Ufaransa, Kwani pande zote zimekubaliana kua beki huyo atasalia klabuni hapo na upande wa mchezaji umekubali ofa ya klabu.
Klabu ya PSG inaelezwa kumpa mkataba wa miaka mitatu beki huyo ili aweze kusalia ndani ya klabu hiyo mpaka mwaka 2027, Kwani beki huyo mkataba wake unamalizika klabuni hapo mwaka 2024 mwezi Juni hivo wakimuongeza miaka mitatu atasalia klabuni hapo mpaka mwaka 2027.
Beki Marquinhos mpaka ndio mchezaji aliedumu ndani ya klabu hiyo kw amuda mrefu kuliko yeyote akiwa amedumu klabuni hapo kwa mwaka wa 10 sasa, Kwani beki huyo alijiunga na klabu ya PSG mwaka 2013 akitokea klabu ya As Roma ya nchini Italia.
Marquinhos amekua mchezaji muhimu ndani ya klabu ya PSG tangu alipojiunga na klabu hiyo kutoka AS Roma mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 19 tu, Lakini mchezaji huyo ameendelea kua mchezaji muhimu ndani ya timu hiyo na ndio chachu ya klabu ya PSG kumuongezea mkataba beki huyo wa kimataifa wa Brazil.