Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marek Hamsik: SSC Napoli wamekosea mahala

Mrek Hamsik Nahodha wa zamani wa SSC Napoli Marek Hamsik

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: Dar24

Baada ya kuutema Ubingwa wa Ligi Kuu ya Italia ‘Sirie A’ mikononi mwa Inter Milan, Nahodha wa zamani wa SSC Napoli Marek Hamsik anaamini Uongozi wa klabu hiyo utafanya usajili mkubwa mwishoni mwa msimu huu.

Inter Milan mwanzoni mwa juma hili ilitwaa Ubingwa wa Ligi kuu ya Italia ‘Sirie A’ baada ya kuichapa AC Milan 2-1, wakimaliza utawala wa SSC Napoli ambao hawakuwa na msimu mzuri.

Gwiji huyo wa soka nchini Slovakia anaamini kuna makosa kadhaa yalifanyika klabuni hapo na kupelekea SSC Napoli kuutema ubingwa wa Sirie A, ambao waliupata baada ya kusota kwa zaidi ya miaka 100.

Amesema anaamini viongozi wamejifunza kutokana na mapungufu yaliyojitokeza, hivyo kila kitu kitakaa vizuri msimu ujao ambao anaamini utakuwa bora kwa klabu yake hiyo ya zamani.

Hamsik, ambaye nusura ajiunge na wafanyikazi wa kocha wa muda Francesco Calzona, ameiambia Sportitalia kuwa: “Sote tumeona kwamba wametatizika mwaka huu.

“Mabadiliko ya makocha watatu katika msimu huu yanamaanisha kuwa mambo hayaendi inavyopaswa na klabu imeelewa hili.

“Nina hakika, kwa sababu hii, watafanya kila linalowezekana kufanya vizuri mwaka ujao, hata kufanya manunuzi kwenye soko. Hasa kwa sababu moja ya nguzo itaondoka, kama (Piotr) Zielinski.”

Hamsiki aliitumikia SSC Napoli kuanzia mwaka 2007 hadi 2019, ambapo alicheza michezo 408 na kufunga mabao 100.

Baada ya kuondoka SSC Napoli, Hamsiki alijiunga na Dalian Professional (2019–2021), IFK Göteborg (2021) na Trabzonspor (2021–2023).

Klabu nyingine alizozitumikia ni Slovan Bratislava (2002–2004) na Brescia (2004–2007).

Chanzo: Dar24