Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marefa waangushiwa jumba bovu

Marefa Kenya Marefa waangushiwa jumba bovu

Thu, 22 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kidole cha lawama kimeelekezwa kwa baadhi ya waamuzi waliyochezesha mechi za Ligi Kuu Kenya mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kocha wa FC Talanta, Ken Kenyatta, alishangazwa na idadi kubwa ya dakika zilizoongezwa kipindi cha kwanza katika mechi waliyopoteza mabao 4-2 mikononi mwa Kakamega Homeboyz.

Katika mchezo huo uliyopigwa Uwanja wa Bukhungu kaunti ya Kakamega, mabao matatu kati ya manne ya Homeboyz yalifungwa kwa mikwaju ya penalti yote yakiwekwa kambani na Michael Karamor.

“Kiwango cha uchezeshaji kilikua cha ovyo. Inakuaje refa anaongeza dakika 16 katika kipindi cha kwanza wakati hakukuwa na majeruhi au ishara zozote za wazi za kupoteza muda.

Penalti nazo hazikuwa sahihi na tunahisi uchezeshaji mbovu ndiyo umetugharimu,” alinukuliwa kocha Kenyatta.

Naye kocha wa AFC Leopards, Patrick Aussems, anaamini kikosi chake kilistahili kupewa mpira wa adhabu kabla Posta Rangers hawajapata bao.

Cavin Odongo aliyeingia kipindi cha pili akitokea benchi, alionekana kumpora mpira beki wa Ingwe, Kayce Odhiambo, kabla ya kuelekea kufunga huku kipa Levis Opiyo asijue cha kufanya.

“Ni timu moja tu ndiyo ilikua inacheza kipindi cha pili na tulijua watacheza mipira mrefu na mwishowe walifunga kwa kucheza counter attack ambapo kwangu mimi ilikua faulo kwa Kaicy,” alisema Aussems.

Aidha wachezaji wa Nairobi City Stays walichelewesha mkwaju wa penalti waliyopewa Nzoia Sugar kupigwa wakilalamika haukutolewa kihaki kufuatia Rowland Makati wa City Stars kumuangusha ndani ya boxi straika Joseph Mwangi.

Chanzo: Mwanaspoti