Katika kuhakikisha wanapunguza makosa na lawama juu ya waamuzi, kamati ya mashindano ya Mapinduzi imeweka wazi kwamba inafikiria kuita waamuzi kutoka nje ya Tanzania kwa ajili ya kuchezesha mashindano hayo.
Kamati hiyo iliweka wazi mpango wake huo kupitia katibu wao mkuu Nasra Juma aliyefanya mahojiano na gazeti la The Citizen jana.
Nasra aliweka wazi kwamba wanafikiria kuchukua waamuzi kutoka Rwanda, Burundi, Sudan na Tanzania bara.
Mpango wa kuchukua marefa nje umekuja ikiwa siku chache tangu Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi wa visiwani Zanzibar Waziri Shekha kuweka wazi kwamba mwamuzi wa mchezo kati ya Simba na Singinda Big Stars Nasri Siyah alifanya makosa kwa kuipa Simba kona ya dakika za mwisho.
Nasra amesema kwamba wanaamini kuchukua waamuzi kutoka nje itapunguza makosa kwenye mashindano hayo.