Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marefa Ligi Kuu wamwibua mwamuzi 'mbabe'

Waamuziiis Marefa Ligi Kuu wamwibua mwamuzi 'mbabe'

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwamuzi ‘mbabe’ wa zamani wa soka hapa nchini, Idd Ngongite amesema amekuwa akisikitishwa sana na makosa wanayofanya marefa kwa sasa Ligi Kuu lakini akakumbuka ingekuwa kipindi cha nyuma ambacho mashabiki na wachezaji walivyokuwa watata  basi kazi ingekuwepo.

Sasa kumekuwa na mijadala mbalimbali inayoendelea mtaani na kwenye mitandao ya kijamii wakiwalalamikia waamuzi juu ya makosa wanayofanya kwenye mechi za Ligi Kuu na kufanya wengi wao kujiuliza wanafanya makusudi au hawafahamu sheria.

Kwa wasiomfahamu Ngongite ni mwamuzi mtemi wa zamani wa soka ambaye alitamba mwanzoni mwa miaka ya 70 kisha akastaafu mwaka 1992 na baadaye akawa mkufunzi wa marefa ambapo kwa sasa amepumzika kutokana na umri kuwa mkubwa.

Ngongite amesema kwanza hafurahishwi na makosa ya kizembe yanaendelea kwa waamuzi lakini pia amewapongeza sana mashabiki, wachezaji wa sasa kwa kuwa wastaarabu na wenye kufuata taratibu na kanuni za soka zilizowekwa na mamlaka.

“Zamani kulikuwa na mashabiki, wachezaji watata sana wewe mwamuzi ukifanya makosa ujue kazi unayo, usipokuwa mbabe basi watakutandika hawakuwa na subra kabisa lakini kwa sasa niwapongeze wamekuwa waungwana sana.

“Sasa ukiangalia matukio wanayofanya waamuzi wetu unabaki unasikitika sana unajiuliza ingekuwa miaka ya 90 unafanya uzembe huu ingekuaje,zamani ukiharibu tu basi ujue watakufuata hadi nyumbani yaani ilikuwa kizaazaa,” amesema.

Ngongite ambaye pia alishawahi kuwa mkufunzi wa marefa, amesema kinachotakiwa kwa sasa ni kuwapa waamuzi mafunzo ya mara kwa mara ambayo yatawajengea uwezo mkubwa kwenye kutafsiri sheria.

“Uzuri kila mkoa kuna chama cha waamuzi hivyo ingekuwa kila baada ya miezi kunakuwa na mafunzo na lengo lake ni kuwajenga kuliko ilivyo sasa wao wanaangalia zaidi mazoezi ya utimamu kuliko kujifunza zaidi kutafsiri sharia,” amesema mwamuzi huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live